spinning heart gifKaribuspinning heart gif

If you want to experience this website in English... I suggest you use the Chrome browser and the translate website tool.
Vinginevyo, jiburudishe...

Utapata nini katika tovuti hii?

Tovuti hii imeundwa nami N Kyalo. Na sina kitu kimoja cha kipekee ningependa kufanya na tovuti hii ila kuitumia kama pahala pangu pa kipekee kwenye mtandao.
Nitaongeza mengi hapa muda ukisonga na nina matumai ya kwamba nitaweza kupenda kazi nitakayoifanya hapa.
Kwa sasa, furahia sanaa yangu, maoni yangu ya vitabu mbalimbali na maandishi yangu.

Mchoro wangu nilioweza kuuchora hivi karibuni

Kwa sasa ninachora kwa mkono kwenye kitabu halafu ninichukua picha ya mchoro huo na kamera ya simu yangu.
Niwie radhi kama ubora wa michoro yangu unakuudhi
Unwaza ona zaidi hapa

Mchoro wa Black Cat, Marvel.
Mchoro wa Black Cat, Marvel Comics.
Mchoro wa Darkchylde.
Mchoro wa Darkchylde

Maoni ya vitabu nilivyovisoma

Nilipenda hadithi kutoka niwe mchanga. Nilionelea heri kusoma riwaya kuliko vitabu vya mtaala/silabasi nilipokuwa shule ya upili.
Hii ni kwa sababu maisha shuleni ilikuwa ya kuhuzunisha kwani nilikuwa katika shule ya bweni.
Na basi nilitaka kuhisi ni kama nina uhusiano na maisha ya nje. Simu zilikuwa haramu shuleni na hata kama hazingeuwa, bado singekuwa nayo kwani babangu hangeninunulia.
Na hapa ndipo nilipoanza kupenda riwaya. zilikuwa zanisaidia kupunguza wwazimu wa kufungiwa shuleni miezi bin miezi.
Mapenzi yangu ya riwaya yalipotea kiasi nilipomaliza shule ya upili. Kwani sikuhitaji maburudisho ya riwaya tena. Nilikuwa na mtandao.
Nayo mtandao wenyewe ukawa wa kuhuzunisha kwani nimeyaona mengi na hakuna kinachonipendeza tena.
Ndivyo nikaja nikapatana na "booktube". Na nikapenda jinsi watu walipata furaha kwa usomaji wa vitabu.
Nmai nikaamua ni muda wangu wa kurudi kwa penzi langu la kale, fasihi.
Hapa utapata jedwali ya vitabu nilivosoma na miezi na miaka nilivyovisoma.
Utagubdua ya kwamba nimeweza kusoma kitabu kimoja tu kila mwezi... Ninag'ang'ana niwezavyo...😔
Fuata viungo kwenye jina ya vitabu hivyo na utaweza kujua maoni yangu ya vitabu hivyo.

Maandishi yangu

Nina nia ya kuandika pia. Si kusoma pekee. Lakini ninahadithi moja tu ambayo ningependa kuandika kitambo niiage dunia, Kyalo.
Basi nimekuwa nikijiambia ya kwamba sihitaji kubuni hadithi nyinginezo kwani hata mimi mwenyewe ninaogopa eti sitazipenda.
Ni jana tu, mnamo 16 wa Oktoba, 2025, nilipoamua hakuna haja ya kuogopa kuandika hadithi nyinginezo zisizokuwa Kyalo.
Hadithi hizi zinaweza kunisaidia mimi mwenyewe niwe msimuliaji bora zaidi.
Nitazichapisha hapa mikipata nafasi na nguvu.
Na tafadhali, usiziibe... Tafadhali!!!