Nina tabu kuita hii hakiki kwani ninawasilisha maoni yangu tu kuhusu
kutabu chenyewe.
Nimefurahi sana kwani nimeweza kukimaliza kitabu changu cha kwanza kwa
muda mrefu sana, miaka hata. Na nimeweza kukimaliza kitabu hiki kwa
mwezi mmoja. Nilivutiwa na kitabu hiki. Mimi si shabiki wa ufalme wa
Kirumi au kitu chochote cha Kirumi.
Ndio maana nilishangaa nilipopata ya kwamba nilikuwa nafurahia kitabu
hiki. Kitabu chenyewe kiliniteka kwa mafumbo yake ambayo kwa bahati
mbaya, hayakutatuliwa mwanzo kitabu kiliisha. Bado nina maswali mengi.
Nilikuwa na tatizo la kutazama akilini kile nilikuwa nikisoma.
Hii nimepata ni shida yangu na si ya kitabu kwani nilisoma uhakiki wa
mtu mwingine aliyependa jinsi mwandishi aliandika. Wengi wamesifia
nathari ya mwandishi ni nimeachwa nikiponda shida yangu ni ipi.
Labda ni kwa sababu imekuwa muda mrefu tangu nikishike kitabu, labda
ni kwa sababu sikujua ya kwamba nina tatizo la kutazama akilini
nisomacho, sijui.
Ninaweza sema ya kwamba mhusika mkuu amezidiwa nguvu kwani hakuna
kilichomshinda. Kila mara alikuwa na vidonda. Sidhani hiyo ni shida,
lakini hiyo ni kuonyesha maisha yake yangekuwa yameisha mara kadha
katika hadithi hili. Hakuna asichojua.
ambapo itabidi asaidiwe, lazima jambo litokee ndiposa aweze kuonyesha
nguvu zake, akili zake, au vyote viwili. Yeye sio mdhaifu kwa
chochote. Hakuna jambo mpya kwake.
Vikwazo vyake vilitokea kwa wengine. Si yeye. Alisemekana kua na shida
za hasira kitabu kilipoanza. Lakini halikuwa tatizo tena alipojua
hasira haitamsaidia. Na sisemi ya kwamba ningependa kumwona akiwa na
hasira kila mara. La hasha!
Yeye kuwa wa asili ya kifalme na kuwa alifunzwa mengi utotoni inahisi
kama njia ya urahisi kwa upande wa mwandishi. Sikumchukia mhusika mkuu
huyu. Lakini sikumpenda pia. Sidhani ninaweza penda mhusika kama yeye.
Nilipenda kitabu hiki licha ya yote niliyoyasema.
Ninajua chuki ya ushoga upo kwenye kitabu hiki lakini ningependa
Eidhin asemekane kuwa shoga siku zijazo. Nimempenda mhusika huyu mno
ingawa alisema machache zaidi kitabu mzima.