Kilichotasfiriwa na Humphrey Davis.
Onyo... unyanyasaji wa kingono kwa watoto, misimamo mikali ya kidini
ya Kiislamu, mateso ya kingono, ubaguzi wa rangi....
Niliamua kusoma kitabu hiki baada ya kutizama video ambayo ilikuwa
inazungumzia vitabu vya Kiafrica vilivyozungumzia haiba ya ujinsia
moja. Na basi nilivutiwa zaidi baada ya kugundua kwamba kitabu hiki
kiliandikwa na mwandishi kutoka Misri. Nilitaka kujua mfumo wa mawazo
ya mhusika yeyote shoga katika kitabu hiki. Shoga huyu ni Hatim
Rasheed. Naye, ni miongoni wa wahusika wakuu lakini si wa maana vile.
Kama mwandishi angeamus kumtoa kwenye kitabu, tofauti ingekuwa ni
ukubwa wa kitabu tu. Hii si kusema ya kwamba sioni umuhumu wake. La
hasha! Misuko ya wahusika wengine wengi wakuu haikutani kamwe. Lakini
ningependa vinginevyo. Hadithi yake Hatim si ya kupendeza. Mara si
kunyanyaswa kingono akiwa mtoto (Na hapa ndipo nilidhani ya kwamba
mwandishi alikuwa mwenye maono eti ushoga ni matokeo ya unyanyasaji wa
ngono kwa watoto. Haikuwa ngumu kufikiria hivi kwani Hatim ndiye shoga
pekee tunayefuata ambaye anataka mahusiano na wanaume wengine.
Ninashuku Abd Rabbuh si shoga. Yeye ni malaya tu kwa Hatim. Lakini
nilibadilisha maono yangu kwa sababu mwandishi aliandika ngono kati ya
Hatim na Abd kwa urembo. Urembo ambao haungekuwepo kama mwandishi
alifikiria ushoga kama zinaa.), mara si mapenzi na mtu ambaye hamtaki.
Mara anaishi maisha yake akimtafuta yeyote anayefanana na yule
mfanyakazi ambaye alimnyanyasa akiwa bado mchanga. Kusoma hadithi yake
ilikuwa ngumu kwani ilikuwa rahisi kutabiri kitakachomtokea. Lakini
Hatim alikuwa kipofu mkubwa sana. Nilimpenda Zaki Bey japo si sana.
Kwani alijiona bila laumu ila alimdhulumu mfanyikazi wake Abaskharon.
Japo hakumtendea mabaya mno, nilisumbuka kila mara hakuona makosa yake
kwani alidhani hivyo ndivyo wafanyakazi hushughulikiwa. Silalamiki eti
aliweza kupata mwisho mwema, la hasha, kwani nilipenda ambavyo hadithi
ya Busayna iliweza kuisha. Busayna ndiye mhusika nimpendaye zaidi kwa
kitabu hiki. Na nina furaha kwa sababu aliweza kupata alichotaka. Naye
Taha el Shazli, niseme nini jameni? Kwa kuwa mwanafunzi mwerevu,
alikuwa mwanaume mpumbavu sana. Huyu ni mwengine niliona mwisho wake
kutoka mbali. Na ni mwisho ambao niliweza kuufurahia ingawa
ninasumbuka nikifikiri anafikiria vivyo hivyo.h!! Souad Gaber!!!
Mhuski wa kusikitisha mno katika kitabu hiki. Mwanamke mwenye ujasiri
na hodari. Sikupenda mwisho wa hadithi yake hata kidogo. Ningependa
mwisho wake uandikwe upwa kama hiyo ni haki niliyokuwa nayo. Cha
kusikitisha zaidi ni ya kwamba sikuridhika na mwisho wa hadithi yake
Hagg Muhammad Azzam hata kidogo. Ndiyo, alidharauliwa kitabu
kilipokuja kuisha, ndiyo, alihisi vibaya. Lakini hiyo hailingani na
robo ya yale Souad aliyoyapitia kwa sababu yake. Hiki ni kitabu
kilochojaa kinaya. Mara si waumini kuwa wafisadi, mfano Hagg 👀.
Nilipenda kitabu hiki. Kilinionyesha mengi sikuyajua kuhusu Misri na
wananchi wake. Na kilinionyesha maisha ya wanamisri kadhaa na jinsi
ufisadi serikalini inavyowaathiri. Niliweza kuona jinsi uhusika wa
Misri na nchi mbali mbali ilivyo. Niliona ndoto za wanamisri na jinsi
jamii ya kimisri huwa. Hiki ni kitabu kilichonionyesha mengi na
ninafuraha nilikisoma. Sentensi zake ni refu kuliko kiasi na bado
ninawaza kama hivyo ndivyo sentensi za Kiarabu huwa...